Jumuiya ya Wafanyakazi wa Migodi na
Ujenzi Afrika Kusini leo imeanza mgomo mkubwa katika sekta ya madini ya
platinamu na hivyo kusimamisha shughuli katika migodi ambayo inazalisha
nusu ya platinamu duniani.
Wafanyakazi wameanza mgomo katika migodi
ya Anglo American Platinum, Impala Platinum and Lonmin na hivyo
kusitisha uzalishaji wa platinamu ambayo ni muhimu katika vipuri vya
magari. Msemaji wa Jumuiya ya Wafanyakazi wa Migodi na Ujenzi Jimmy Gama
amesema mgomo huo umesitisha oparesheni zote katika migodi. Jumuiya
hiyo ina wanachama 100,000 wanaofanya kazi katika 'ukanda wa platinamu'
yapata kilomita 120 kutoka Johannesburg. Wafanyakazi waliogoma wanataka
nyongeza maradufu ya mshahara wa awali huku wenye migodi wakisema
watatoa nyongeza ya asilimia 7.5 hadi 8.5. Ikumbukwe kuwa mwaka 2012
kulikuwa na migomo katika migodi hiyo ambapo makumi ya watu waliuawa.
Inaelezwa kuwa, aghlabu ya mashirika
katika sekta ya madini nchini Afrika Kusini yanamilikiwa na Wamagharibi
ambayo licha ya kupata faida kubwa sana katika uwanja huo lakini
yamekuwa yakiwalipa mishahara duni wafanyakazi wao.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!