Kesi inayowakabili wanaume wanne
wanaotuhumiwa kuhusiana na shambulio la al-Shabaab kwenye kituo cha maduka ya
biashara ambalo liliwaua watu wapatao 67 mwezi Septemba mwaka uliopita
ilifunguliwa Jumatano (tarehe 15 Januari) huko Nairobi, AFP iliripoti.
Wanaume hao -- Adan Mohamed Abidkadir Adan, Mohamed Ahmed Abdi, Liban Abdullah Omar na Hussein Hassan Mustafah -- wanatuhumiwa kwa kutoa msaada kwa wanaume wenye silaha ambao walivamia kituo hicho cha biashara. Wote walikana mashtaka hayo.
Wanaume wote hao waliokuwa na silaha katika uzingiraji wa Westgate waliaminika kuwa walikufa wakati wa shambulio hilo. Shirika la Kimataifa la Polisi la Makosa ya Jinai na Shirika la Upelelezi la Marekani yalisaidia Kenya katika kujaribu kutambua miili minne inayoaminika kuwa ya washambuliaji hao.
Hata hivyo, ripoti ya polisi wa New York ya mwezi uliopita ilionyesha kwamba washambuliaji walitoroka.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!