Mamia ya Wasomali husimama kwenye mistari mirefu kila siku kwenye kituo
pekee huko Mogadishu ambacho kinatoa kadi za utambulisho, na mara nyingi
siyo kutoka kwa mtu mmoja utasikia malalamiko kuhusu ugumu na muda
mrefu unaotumiwa katika mchakato huo.
Kituo hicho kilifunguliwa hivi karibuni tarehe 23 Desemba kwenye eneo la bandari ya zamani katika wilaya ya Abdulaziz.
Kusaidia kuhudumia mahitaji makubwa, utawala wa mkoa wa Benadir ulisema unapanga kufungua vituo vya ziada mahali pengine huko Mogadishu, lakini tahadhari itachukua muda kukamilika.
"Tunajua kwamba kituo cha kutoa vitambulisho tulichokifungua kina msongamano mkubwa na zaidi ya watu 500 wanakuja kwenye kituo hiki kila siku," msemaji wa utawala wa Benadir Mohamed Yusuf alisema. "Tunapanga kufungua vituo vingine katika wilaya nyingine za Mogadishu, lakini bado tunafikiria kuhusu muda unaofaa kuvifungua."
Alisema serikali ya shirikisho inapanga kuwa na vituo vya uendeshaji katika kila wilaya ya Somalia ifikapo mwishoni mwa 2014.
"Kufungua vituo vingine sio kazi ambayo inaweza kukamilika katika siku moja au mbili," alisema. "Kunatakiwa kuwa na mchakato ulioboreshwa na idara zote zinazohusika katika usimamiaji wa data na utoaji wa vitambulisho kuweza kufanya kazi pamoja kupitia mfumo mmoja wa kompyuta."
Kitambulisho cha alama za kibiolojia kinatakiwa kwa raia wanaotaka kupata pasipoti mpya ya Somalia. Pia kinatakiwa katika kununua ardhi na magari, kufungua akaunti ya benki, kujiandikisha chuo kikuu, kusafiri ndani ya Somalia kwa ndege, na kuthibitisha utambulisho wa mtu katika vituo vya ukaguzi vya usalama katika mji wote.
Kimsingi, kitambulisho kinagharimu Dola 10.50, pamoja na Dola 5 nyingine ili kupata cheti rasmi cha kuzaliwa. Kuanzia Januari 2014, gharama imeongezeka kwa Dola 2. Yeyote anayetaka kitambulisho anatakiwa kulipa ada ya Dola 17.50 moja kwa moja kupitia Benki ya Dahabshiil au ya Salaam.
Kila mwombaji lazima atoe alama za vidole, picha na kuchunguzwa kama alishafanya uhalifu, Yusuf alisema. baada ya kuwasilisha karatasi zote zinazotakiwa, wanaambiwa kurudi baada ya wiki moja kuchukua nyaraka zao.
Lakini hakuna watu waliopata vitambulisho vyao katika muda huo uliopangwa. Ukweli, baadhi ya watu wanaohusika walisema kuwa wamekuwa wakisubiri kwa takribani wiki tatu.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!