MSHAMBULIAJI wa zamani
wa AS Roma ya Italia na Ajax Amsterdam ya Uholanzi, Mido ameteuliwa kuwa
kocha mpya wa klabu yake ya nyumbani ya Zamalek. Mido anachukua mikoba
ya kocha Helmi Toulan ambaye alitimuliwa kufuatia sare ya bao 1-1
iliyopata Zamalek dhidi ya Haras El-Hodood katika mchezo wa Ligi Kuu
nchini Misri. Hiyo inakuwa mechi ya nne kwa Zamalek msimu huu ambapo
klabu hiyo inashika nafasi ya nne baada ya kushinda mechi mbili kutoa
sare moja na kufungwa moja. Mido ambaye anafikisha umri wa miaka 31
Februari mwaka huu anakuwa kocha mdogo zaidi katika historia ya soka
nchini hiyo na hana uzoefu wa kutosha wa kufundisha. Nyota huyo ambaye
alianza kusakata kabumbu Zamalek mwaka 1999 kabla ya kwenda kucheza
Ulaya ameifungia timu ya taifa ya nchi hiyo mabao 19 katika mechi 51
alizocheza.
Home »
michezo africa
» MIDO ATEULIWA KUWA COACH MPYA WA ZAMALEK
MIDO ATEULIWA KUWA COACH MPYA WA ZAMALEK
Written By Unknown on Thursday, 23 January 2014 | Thursday, January 23, 2014
Labels:
michezo africa
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!