Serikali
ya Thailand inasema itatuma maelfu ya maafisa wa usalama kote nchini
kuhakikisha kuwa kuna usalama wakati huu taifa hilo likijiandaa kwa
uchaguzi mkuu siku ya Jumapili. Wachambuzi wa siasa nchini humo wanasema
uchaguzi huo wa jumapili huenda usimalize machafuko yanayoendelea hasa
baada ya upinzani kusema watashirki.
Waandamanaji kwa miezi kadhaa sasa wamekuwa wakimshinikiza
waziri mkuu Yingluck Shinawatra kujiuzulu kutokana na serikali yake
kuendelea kupata ushauri kutoka kwa kaka yake Thaksin Shinawatara ,
shinikizo ambazo amekataa na badala yake kuitisha uchaguzi mkuu.
Nchi ya Thailand imejikuta kwenye hali mbaya kisiasa toka kupinduliwa kwa waziri mkuu wa zamani Thaksin Shinawatra miaka 7 iliyopita na sasa mdogo wake, Yingluck Shinawatra anakabiliwa na shinikizo la kujiuzulu akituhumiwa kuongoza nchi kwa kuzingatia matakwa ya ukoo wake.
Hofu imezidi kutanda nchini humo kufuatia shambulizi la hivi karibuni ambalo ni miongoni mwa matukio mabaya kushuhudiwa tangu kuanza kwa harakati za kuipinga serikali ya Yingluck.
Awali upinzani ulipinga kushiriki kwenye uchaguzi ukihofia ushindi kushikiliwa tena na familia ya Shinawatra.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!