MAMA
wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa ameibuka na kueleza kuwa,
Elizabeth Michael ‘Lulu’ ni mkwe sahihi kwake kwa namna alivyo na
heshima na anavyomjali kama mama yake.
|
Mama mzazi wa marehemu, Steven Kanumba, Flora Mtegoa akipozi na Lulu. |
Akizungumza wikiendi iliyopita nyumbani kwake, Kimara - Temboni, Dar,
mama huyo alisema, kama mwanaye angekuwa hai angekuwa amepata mke bora
wa maisha yake, naye pia alikuwa na mkwe sahihi.“Najua mtoto wangu
ametangulia mbele za haki lakini faraja anayonipa Lulu ni kubwa mno na
najisikia furaha. Kama Mungu angemwacha Kanumba hai mpaka leo kwa kweli
Lulu angekuwa mkwe bora sana kwangu.
|
Elizabeth Michael ‘Lulu’. |
“Sina jinsi, ndiyo imeshatokea lakini mimi kama mzazi bado
nitaendelea kumpenda na kuwa bega kwa bega na Lulu hata akipata mchumba
mwema wa kumuoa, sina tatizo na hilo... namwombea sana kwa Mungu huyu
binti,” alisema kwa hisia mama Kanumba.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!