Home »
news
» RADIO CLOUD'S FM YA TANZANIA YAWATEMA HAWA WATANGAZAJI WAKE WA 3 MAARUFU.
RADIO CLOUD'S FM YA TANZANIA YAWATEMA HAWA WATANGAZAJI WAKE WA 3 MAARUFU.
WATANGAZAJI
maarufu nchini Tanzania wa Redio Clouds Fm ya jijini Dar es Salaam, Hamis Mandi
‘B 12’, Adam Mchomvu na Loveness Malinzi ‘Diva’, wamepigwa chini na
kituo hicho.kwa mujibu wa mtandao wa GP
|
Hamis Mandi ‘B 12’. |
Habari za chini kwa chini kutoka kwa chanzo chetu zinasema kuwa
uongozi wa Clouds umefikia hatua hiyo baada ya kuchoshwa na tabia ya
utovu wa nidhamu wa watangazaji hao.
Hata hivyo, madai ya mitaani yanasema kwamba watangazaji hao
wamepigwa chini kwa kosa la kukacha sherehe za maadhimisho ya miaka 14
ya Clouds FM,yaliyofanyika hivi karibuni katika Viwanja vya Mwembeyanga,
Temeke, Dar.
Mkurugenzi wa Vipindi na
Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba na alipo ulizwa juu ya ishu
hiyo ambapo alikiri.
|
Adam Mchomvu. |
“Ni kweli tumefikia uamuzi wa kuwasimamisha B 12, Diva na Mchomvu
baada ya kukiuka baadhi ya makubaliano baina yao na ofisi hivyo
kusababisha usumbufu mkubwa ambao ulitulazimu kuingia gharama ambazo
hazikutarajiwa.
“Hatutakuwa nao kwa muda usiojulikana ingawa watu wengi wamekuwa
wakinihoji juu ya hilo lakini watachotakiwa kuelewa ni kwamba hakuna
ofisi isiyokuwa na sheria na taratibu za kuongoza watu wake, sasa hao
wamevunja taratibu zetu,” alisema Ruge bila kufafanua zaidi.
|
Loveness Malinzi ‘Diva’. |
Alipoulizwa ni taratibu zipi watangazaji hao walizovunja alisema:
“Nashindwa kueleza kosa la kila mmoja ila naomba nieleweke kuwa hao
watangazaji kwa sasa tumewasimamisha kwa muda usiojulikana wakati
tukifikiria cha kufanya. Muhimu hapo ni kwamba wamekwenda kinyume na
tulivyokubaliana.”
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!