Nchini Libya watu wasiopungua 154 wameuawa katika wiki mbili za
mapigano makali ya kikabila. Wizara ya Afya ya Libya imetoa taarifa siku
ya Jumamosi na kusema watu wengine karibu 470 wamejeruhiwa katika
mapigano hayo ya kikabila katika miji ya Sebha na Wershefana. Sebha ni
mji mkubwa katika eneo la kusini mwa nchi hiyo nao Wersehfana ni mji
ulio magharibi mwa Tripoli. Mji wa Wersehfana ni ngome ya wafuasi wa
dikteta aliyepinduliwa Muammar Gaddafi. Maafisa wa afya wanasema yamkini
idadi ya waliopoteza maisha ni kubwa zaidi. Katika mji wa Sebha
mapigano yaliripotiwa kuwa baina ya makabila ya Toubou na Awled Sleiman.
Tokea dikteta Muammar Gaddafi atimuliwe madarakani mwaka 2011, serikali ya Libya imeshindiwa kudhibiti makundi ya wanamgambo ambao walishiriki katika kumpindua Gaddafi. Aidha wafuasi wa Gaddafi wameanza kujitokeza na kuibua mapigano katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!