Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini amekosoa mpango wa kulinda amani
wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNIMISS na kutuhumu kuwa utendaji wake
ni kana kwamba ni serikali kivuli katika nchi hiyo.Kiir ametoa
matamshi hayo baada ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon
kusema kwamba, maafisa wa ngazi za juu wa serikali ya Juba na wanajeshi
wameripotiwa kuwatishia wafanyakazi wa umoja huo pale walipojaribu
kuingia katika eneo linalowahifadhi maelfu ya raia waokimbia mapigano
linalosimamiwa na UN.
Ban alisisitiza kuwa, vitisho hivyo dhidi ya maafisa wa umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini ni miongoni mwa vipengee vinavyovunjwa kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa kati ya pande mbili suala linaloleta ugumu kwa UNIMISS kutekeleza majukumu yake ipasavyo katika nchi hiyo.
Hayo yanajiri huku mapigano yakiendelea kushuhudiwa kati ya vikosi vya serikali ya Juba na waasi.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!