Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » AMNESTY INTERNATIONAL YAOMBA JELA YA GUANTANAMO KUFUNGWA

AMNESTY INTERNATIONAL YAOMBA JELA YA GUANTANAMO KUFUNGWA

Written By Unknown on Wednesday, 22 January 2014 | Wednesday, January 22, 2014

Shirika la Msamaha Duniani Amnesty International limesema kuwa, hatua ya Marekani ya kuendelea kuendesha jela ya Guantanamo Bay nchini Cuba na kuendelea kuteswa mahabasu wa jela hiyo ni mfano wazi wa mtazamo wa kindumilakwili wa Washington kuhusu haki za binadamu.
Amnesty imesema leo kuwa, kila mwaka Marekani inavyoendelea kuendesha jela hiyo ndivyo inavyoendelea kudhihirisha kutoshikamana kwake na vigezo vya kimataifa vya haki za bindamu na kwamba kama ni nchi nyingine ingekuwa inavunja haki za bindamu kama inavyofanya Marekani huko Guantanamo basi ingelaaniwa na Washington.  Shirika hilo limesisitiza kuwa, wakati umefika sasa wa Marekani kuacha undumilakwili na kufunga jela hiyo ambako mahabusu wake wanashikiliwa kwa muda mrefu, bila kuhukumiwa  huku wakipata mateso makubwa.
Amnesty Internation pia imemkosoa Rais Barack Obama kwa kushindwa kutekeleza ahadi yake ya kufunga jela ya Guantanamo kama alivyoahidi mara tu baada ya kuingia madarakani mwaka 2009. 
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi