Diamond amefunguka ambapo amedai kuwa wazo hilo lilitoka kwenye mitandao ya kijamii kupitia mashabiki wake walitoa mapendekezo ya zawadi atakayopewa mshindi wa shidano hilo.
“Wakati tunafanya lile tangazo, tulitoa katika mitandao tofauti tofauti, nikawauliza wananchi mnafikiri kitu kipi kizuri ambacho mtoto akishinda apewe, lakini mawazo mengi yalikuwa yanakuja kwamba hao watoto tuangalie katika upande wa kielimu zaidi.” Ameeeleza Diamond.
Amesema alichukua wazo hilo na kulipeleka kwenye menejimenti yake ambayo iliona lina maslahi kwa pande zote na kulipitisha.
“Tukafanya hayo mashindano na kweli watoto hao wakatokea wakashinda, kwa hiyo ikawa ni swala la kutafuta ni shule ipi ambayo itakuwa ni bora na nzuri ambayo watoto watapata elimu bora. Tulichokiangalia sisi ni kwamba aliyekuwepo darasa fulani tutamuendeleza kutoka pale kwenda mbele, na mtu akiwa yuko katika shule ambayo sio International basi sisi tutampeleka International.” Diamond amefunguka.
Diamond akisalimiana na mkuu wa shule hilo |
“Unajua tatizo la sanaa, lazima kuna sehemu kwanza inabidi ifikie kwenye level ya kielimu ndipo uanze kumuendeleza kimuziki la sivyo utampotosha asisome kabisa. Hata mimi wakati nasoma nilipomaliza darasa la saba mama yangu aliniambia kwamba wewe soma kwanza muziki utafanya.
Diamond akiwa katika ofisi ya mwalimu mkuu wakati wakuwaandikisha watoto hao |
Diamond na wazazi wa watototo Akiwa ofisini kwa mwalimu |
Watoto waliopata bahati yakusomeshwa na Diamond |
“Na mimi ntasikia raha hata kesho nikisikia mtoto ambaye kasomeshwa akaja kuwa kesho hata kuwa waziri ambapo ule muziki ndio umemfanya yeye kuwa waziri, na sio lazima awe mwanamuziki.”
Kupitia Instagram, Diamond ameshare picha zinazoonesha akiwakabidhi watoto hao katika shule ya kimataifa ‘East Africa International School’ iliyopo Mikocheni mjini Dar es Salaam.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!