Mary Robinson mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa katika eneo la maziwa makuu ya Afrika leo amewasili Kinshasa
mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa shabaha ya kukutana na
viongozi wa ngazi za juu nchini humo.
Taarifa kutoka Kinshasa zinaeleza kuwa, Bi. Robinson atakutana na kufanya mazungumzo na Augustin Matata Ponyo Mapon Waziri Mkuu, Raymond Tshibanda Waziri wa Mashauri ya Kigeni na viongozi wa tume huru ya uchaguzi huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anafanya safari nchini humo zikiwa zimepita siku chache tokea nchi hiyo iliposhuhudia uasi dhidi ya serikali ya Rais Joseph Kabila tarehe 30 Disemba mwaka jana, machafuko yaliyopelekea makumi ya watu kuuawa na mamia ya wengine kujeruhiwa.
Serikali ya Kinshasa ina matumaini kwamba misaada ya kijeshi ya Umoja wa Mataifa inaweza kusaidia mchakato wa kupokonywa silaha makundi yanayobeba silaha katika maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!