KIUNGO Steven Gerrard amesema alipata maumivu ya tumbo ghafla
baada ya kupata ripoti za kuumia kwa staa wa Arsenal, Mwingereza Theo
Walcott na kwamba atakosa fainali zijazo za Kombe la Dunia
zitakazofanyika Brazil.
Wakati Gerrard akikiri kuumizwa na habari hizo,
beki wa kushoto wa Arsenal, Kieran Gibbs alibainisha kwamba Walcott yupo
vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti.
Gibbs alikwenda kumtembelea mchezaji mwenzake huyo hospitalini juzi Jumamosi na kumpa pole baada ya kufanyiwa upasuaji.
Walcott amefanyiwa upasuaji na hatarudi uwanjani
kwa msimu wote, jambo linalomfanya kuwa na nafasi ndogo sana ya kucheza
fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika baadaye mwaka huu.
Walcott atakuwa nje ya uwanja kwa takriban miezi
sita baada ya kuumia kwenye mechi ya Kombe la FA dhidi ya mahasimu wao
wa London, Tottenham Hotspur ambapo Arsenal ilishinda mabao 2-0.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!