Kufuatia ripoti zilizoenea hivi karibuni nchini Kenya
zikidai kuwa ‘Kigeugeu hitmaker’ Jaguar ndiye mshauri wa Rais wa Kenya,
Uhuru Kenyatta kwenye maswala ya yanayohusu vijana, mwimbaji huyo
amekanusha taarifa hizo.
Jaguar ametweet akikanusha taarifa hizo na kudai kuwa safari zake kuitembelea Ikulu ya nchi hiyo huwa na lengo la kumtembelea rais Kenyatta kama rafiki yake.
Mwimbaji huyo ambaye hivi sasa video ya wimbo wake Kioo imeshika vipindi vya burudani vya runinga Afrika Mashariki, amekuwa mstari wa mbele katika kusaidia harakati za kuwainua vijana nchini Kenya.
Jaguar ametweet akikanusha taarifa hizo na kudai kuwa safari zake kuitembelea Ikulu ya nchi hiyo huwa na lengo la kumtembelea rais Kenyatta kama rafiki yake.
.. Articles stating that I'm the President's youth advisor; My visits
to state house are solely to see His Excellency as a personal friend.
— Real Jaguar Kenya (@RealJaguarKenya) January 15, 2014
Akiongea na mtandao wa Ghafla wa Kenya, Jaguar amesema kuwa wakati
wowote ambapo Rais Kenyatta anapohitaji maoni yake kuhusu maswala
yanayowahusu vijana nchini humo, huwa tayari kutoa maoni yake.Mwimbaji huyo ambaye hivi sasa video ya wimbo wake Kioo imeshika vipindi vya burudani vya runinga Afrika Mashariki, amekuwa mstari wa mbele katika kusaidia harakati za kuwainua vijana nchini Kenya.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!