Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » HATIMAYE MATOKEO YA KURA YA MAONI NCHINI MISRI YATANGAZWA

HATIMAYE MATOKEO YA KURA YA MAONI NCHINI MISRI YATANGAZWA

Written By Unknown on Thursday, 16 January 2014 | Thursday, January 16, 2014

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Misri ametangaza kuwa, zaidi ya asilimia 55 ya Wamisri waliotimiza masharti ya kupiga kura walishiri katika kura ya maoni ya katiba mpya na pengine asilimia 95 kati yao wamepiga kura ya ndio.
Katika hali ambayo duru za habari zimejiepusha kutangaza kiwango cha ushiriki wa wananchi kwenye zoezi hilo, maafisa wa Cairo wamedai kuwa matokeo ya awali ya kura hiyo ya maoni yanaonesha kuwa, kiasi kikubwa cha watu walishiriki kupiga kura. Matokeo rasmi ya kura ya maoni ya katiba mpya ya Misri iliyosusiwa na wapinzani na makundi mengine ya kimapinduzi yanatarajiwa kutangaza siku ya Jumapili.

Zoezi hilo lilifanyika kwa siku mbili mtawalia na kumalizika  jana Jumatano huku kukishuhudiwa ukandamizaji wa waandamanaji waliokuwa wakimuunga mkono rais halali aliyechaguliwa na wananchi na kupinduliwa na jeshi Muhammad Musri. Watu 11 waliuawa na wengine 450 kutiwa mbaroni wengi wao wakiwa wafuasi wa harakati ya Ikhwanul Muslimin.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi