Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » SERIKALI YA IRAN YAPONGEZWA NA KENYA KWA MAKUBALIANO YA GENEVA

SERIKALI YA IRAN YAPONGEZWA NA KENYA KWA MAKUBALIANO YA GENEVA

Written By Unknown on Thursday, 16 January 2014 | Thursday, January 16, 2014

Kenya imeipongeza Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa mafanikio yake ya kidiplomasia hivi karibuni katika mazungumzo ya nyuklia na nchi za 5+1.  Hayo yameelezwa na Spika wa Bunge la Seneti ya Kenya Mh. Ekwe Ethuro  alipofanya mazungumzo na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iran Ishaq Jahangiri.  Katika mazungumzo hayo ya Jumatano jioni mjini Tehran, Ethuro ameelezea matumaini yake kuwa kutekelezwa Makubaliano ya Nyuklia la Geneva na kuondolewa vikwazo dhidi ya Iran kutaandaa mazingira ya ushirikiano zaidi wa sekta binafsi za Iran na Kenya.
Ikumbukwe kuwa Makubaliano ya Nyuklia ya Geneva yalitiwa saini Novemba 24, 2013 kati ya Iran na nchi za 5+1 ambazo zinajumuisha China, Russia, Uingereza, Ufaransa, Marekani pamoja na Ujerumani. Kwa mujibu wa mkataba huo, Iran itapunguza baadhi ya shughuli zake za nyuklia, nayo Marekani na waitifaki wake waiondolee Jamhuri ya Kiislamu baadhi ya vikwazo.
Spika wa Bunge la Seneti la Kenya Mh. Ethuro pia ameashiria uhusiano wa kihistoria wa Iran na bara la Afrika na kusema kuwa safari yake ya siku tano nchini Iran imekuwa ni yenye manufaa.

Kwa upande wake Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iran Ishaq Jahangiri ameipongeza Kenya kwa mnasaba wa kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wake. Aidha amesema sekta binafsi katika uchumi wa Iran ina uwezo mzuri na hivyo serikali inaunga mkono wawekezaji Wairani wanaotaka kuwekeza nchini Kenya. Jahangiri amesema kustawisha uhusiano na nchi za Afrika hasa Kenya ni suala lenye muhimu wa kistratijia kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Ameongeza kuwa tayari kuna mashirika binafsi ya Iran yanayofanya kazi nchini Kenya katika miradi ya kilimo na ujenzi wa vituo vya kuzalisha umeme. Aidha ameashiria uwekezaji wa Wakenya nchini Iran na kusema serikali inajitahidi kuondoa vizingiti vilivyoko katika miradi hiyo ili kuandaa mazingira ya kuboresha zaidi uhusiano wa kibiashara wa Tehran na Nairobi.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi