Baada ya Habari kukaa kwenye midomo ya watu,kwenye mitandao,kwenye vyombo kama vyote vya habari vya hapa Burundi kwa kuizungumzia bifu ya wanamuziki wa wili wenye majina yani maarufu hapa nchini,nawazungumzia wakina nani?nawazungumzia Niyonzima Nassor Salum ama baba Rahma na Mugani Desire ama Burundiano.
Bifu hiyo ambayo hadi sasa habari hii inaandikwa bado yazidi kutokota kama volcano...
Pindi bifu hiyo ikirurumba huku kila fans wa wanamuziki hao akikokota upande wake nakusema mwanamuziki wangu ana haki mwengine hapana mwanamuziki wangu ameonewa yeye ndo mwenye haki,hayo yote yakitokana na nini?yakitokana na kile ambacho kikiwa kama ndo chanzo cha bifu hiyo naizungumzia ile concert ya Ijumapili.
Sat-b na Lolilo |
Sat-b na Burundiano baada yakutoka kwenye bifu |
Sat-b ameonekana kuvunja ukimya wake nakutowa yamoyoni ambayo yameonekana kumlenga umoja mwa wawili hao wenye bifu namzungumzia Lolilo.
Hadi sasa hakujawa na sababu haswa za mwanamuziki Sat-b kumtolea mbovu Lolilo na ilhali hawana ubaya.
Sat-b ameonekana kumlenga zahiri mwanamuziki Lolilo kwenye post hiyo aliyo iangusha kwenye mtandao wa facebook.
Lolilo ambae ni Star wa Africa mashariki na rafiki wa karibu na tajiri na mmiliki wa My number one rmx namzungumzia Nassib Abdul Djuma a.k.a Diamond.
Kwenye post hiyo kunasomeka maneno yasemayo hivi "lazima achapwe rungu hata kama ni mkubwa" huku akitaja na jina.
Wachambuzi wa karibu wa habari wameweza kutowa uchambuzi wao kuhusiana na kauli hiyo ambayo ameiandika jana mwanamuziki huyo kwenye mtandao wa facebook,eti Sat-b kuandika kitu hicho nimfano wa mtu anae iona nyumba ya nyasi ya jirani yake ikiwaka kisha na yeye anasogeza majani.
Bimana ameujikokotea moto ambao ameutowa kwa Burundiano nakuuweka kwake.
Sat-b hivi karibuni alionekana kutowa onyo kwenye Redio Rema fm kwenye kipindi cha Changamka show alipo pigiwa sim na mwanahabari anae ongoza kipindi hicho Mh Ismail Niyonkuru nakusema kuwa atakae taka kufanya bifu na yeye basi yeye yupo tayari na akaongeza kuwa yeye hatomchapa kwa fimbo bali kwa maneno kwa sababu mashahiri anayo na wala si yakuogoteza ogoteza yani yakuunga unga.
Je,unahisi Lolilo atavumilia haya ambayo anayo zidi kutendewa na wanamuziki wa Burundi tukijumuisha yanayo endeleya kati yake na Burundiano ambayo hayajakwisha na yangine yanakuja,hususani tukifata kwa makini ile kauli aliyo itamka kuwa kwanini anapenda kuonewa? na kuongeza tena na hiki ambacho mwanamuziki Sat-b amemchana kwenye mtandao.
Je,unahisi Lolilo ataihamisha bifu kwa Sat-b akiitowa kwa Burundiano?tusubiri tuone ila ningependa kukwambi kuwa mapema leo Sat-b alikuwa amesha iondowa post hiyo hata ukiitafuta hauwezi kuipata ila mtandao wako uliinasa mapema na ukaona ni vyema mwenyewe uijisomee post hiyo mjisomee wenyewe vile Sat-b alivyo mchana Lolilo akimwambia lazima achapwe rungu kwa kuwa amekosa adabu.
Soma ndo hiyi hapa:
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!