Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » RAIA WA LIBYA WAMEINGIA BARABARANI NA KUANDAMANA KWA KUPINGA MACHAFUKO

RAIA WA LIBYA WAMEINGIA BARABARANI NA KUANDAMANA KWA KUPINGA MACHAFUKO

Written By Unknown on Monday, 13 January 2014 | Monday, January 13, 2014

Wakazi wa mji wa Benghazi nchini Libya wamefanya maandamano makubwa wakipinga machafuko, ukatili ma mauaji yanayoendela kufanyika katika mji huo wa mashariki mwa Libya.
Waandamanaji hao wamelaani pia vitendo vya kutekwa nyara raia, na ukosefu wa amani na wameitaka serikali ya Tripoli kufanya jitihada kubwa za kulinda usalama wa raia.
Mji wa Benghazi ambao ndiyo kitovu cha mapinduzi ya wananchi wa Libya yaliyomuondoa madarakani dikteta wa zamani wa nchi hiyo Muammar Gadafi tarehe 17 Februari mwaka 2011 kwa muda sasa umekumbwa na machafuko na mauaji yanayowalenga raia na askari na vilevile utekaji nyara.
Ripoti za hivi karibuni zinasema kuwa zaidi ya watu 200 wameuawa katika machafuko ya sasa ya Benghazi wengi wao wakiwa shakhsia wa kisiasa, wanajeshi na wasomi.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi