Siku kama ya leo miaka 35 iliyopita kulitokea mapigano
makali kati ya maafisa wa utawala wa Shah na wananchi wa Iran ikiwa ni
wakati yalipofanyika maandamano makubwa ya wananchi katika miji kadhaa
ya Iran. Wananchi wengi wanamapambano waliuawa shahidi na wengine
kujeruhiwa katika maandamano hayo. Katika siku hiyo pia wanachuo na
wakazi wa mji wa Tehran ambao walikuwa wamekusanyika kwa wingi mbele ya
Chuo Kikuu cha Tehran walitangaza kuupinga utawala wa Shah wakitaka
kurejea Tehran Imam Khomeini M.A, kutoka Paris, Ufaransa. Harakati hiyo
ya wanafunzi wa vyuo vikuu ilishuhudiwa huku maeneo ya vyuo vikuu
yakizingirwa na wanajeshi na vikosi vya usalama.
Miaka 73 iliyopita katika siku kama leo ulifanyika huko
London, Uingereza mkutano wa kihistoria wa waitifaki wa Ulaya wakati wa
Vita vya Pili vya Dunia. Mkutano huo ulifanyika kufuatia pendekezo
lililotolewa na Winston Churchill, waziri mkuu wa zamani wa Uingereza
kwa lengo la kuratibu siasa za viongozi wa nchi za Ulaya katika medani
za vita dhidi ya nchi mbili za Ujerumani na Italia. Mkutano huo
ulihudhuriwa na Uingereza, Uholanzi, Ubelgiji, Ufaransa, Ugiriki,
Norway, Luxembourg na Denmark.
Na miaka 564 iliyopita katika siku kama ya leo, alizaliwa
Bartholomeo Dias baharia na mvumbuzi wa Kireno. Baada ya kukatisha
Bahari ya Atlantic kuelekea upande wa kusini, mwaka 1488 Miladia Dias
alivumbua Rasi ya Tumaini Jema (Cape of Good Hope) katika ncha ya kusini
zaidi ya bara la Afrika. Miaka 10 baadaye Vasco da Gama baharia
mwingine wa Kireno alifanikiwa pia kuvumbua njia inayokwenda hadi India
kupitia masafa hayo hayo ya Afrika.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!