Akihutubia wananchi wa Rwanda hapo jana na kuzungumzia mauaji yaliyofanywa dhidi ya Kanali Patrick Karegeya mkuu wa zamani wa Idara ya Upelelezi ya nchi hiyo, Rais Kagame ameongeza kuwa, watu wanaofanya vitendo vya uhaini wanapaswa kukabiliwa na adhabu kali. Rais wa Rwanda amesisitiza kuwa, hatakubali kuona matunda yaliyopatikana kutokana na juhudi zilizofanywa na wananchi wa nchi hiyo kwa miaka kadhaa, yakioharibiwa na baadhi ya mahaini.
Mwanzoni mwa mwaka huu, kilitangazwa kifo cha Kanali Patrick Karegeya ambaye inasemekana aliuawa hotelini nchini Afrika Kusini. Kwa muda wa muongo mmoja, Kanali Karegeya alikuwa mkuu wa Idara ya Upelelezi ya Rwanda, na pia alikuwa mtu wa karibu kwa Rais Kagame. Uhusiano wa viongozi hao wawili ulianza kuingia dosari baada ya Kanali Karegeya kumuita Kagame kuwa ni dikteta na hatimaye kutorokea nchini Afrika Kusini mwaka 2007.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!