Wananchi wa Marekani wameandamana katika miji mbalimbali ya nchi hiyo wakiitaka serikali ya Rais Barack Obama ifunge jela ya Guantanamo Bay na kuwaachia huru mahabusu ambao hawajapatikana na hatia yoyote.
Makumi ya waandamanaji walikusanyika mbele ya Ikulu ya White House mjini Washington hapo jana sambamba na kuadhimishwa mwaka wa 12 tangu mahabusu wa kwanza walipopelekwa kwenye jela hiyo ya Marekani nchini Cuba. Maandamano kama hayo yameshuhudiwa pia katika miji ya Miami, Santa Monica na Chicago.
Charles Abbot kutoka Kitengo cha Uadilifu na Sheria za Kimataifa aliyeshiriki maandamano hayo amesema, wanakumbuka mwaka wa 12 tangu kufunguliwa jela yenye kutia aibu ya Gunantanamo, inayodhihirisha ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa.
Mwaka 2008 wakati wa kampeni zake za uchaguzi Rais Barack Obama aliahidi kuifunga jela hiyo lakini suala hilo hadi leo halijatekelezwa
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!