BEKI wa zamani wa Brazil na Real Madrid, Roberto Carlos, amekaa
dakika chache na wachezaji wa Yanga mjini Antalya, Uturuki na kuwapa
somo la maana.
Roberto Carlos |
Gwiji huyo anayeheshimika kwa mafanikio yake
aliyoyapata akitumia mguu wa kushoto, alishituka baada ya kusikia Yanga
inatoka Tanzania ambako aliwahi kufundisha Kocha Mbrazili, Marcio
Maximo, ambaye yeye anamheshimu sana.
Carlos alipiga picha na wachezaji wa Yanga halafu
baadaye yeye na timu yake wakaangalia mazoezi ya wana Jangwani hao kwa
dakika kumi kisha akakaa nao na kuzungumza kidogo na kuwachangamkia.
“Nimefurahi sana kusikia kwamba mmetoka Tanzania
alikokuwa anafundisha Maximo (kocha wa zamani wa Taifa Stars),
ninamheshimu sana yule kocha,” aliwaambia wachezaji wa Yanga.
“Ni katika watu muhimu sana kwangu, wachezaji
nimewafurahia mnavyocheza. Mnachotakiwa kufanya ni kuongeza juhudi
mkitambua kwamba kila mmoja ana nafasi yake ya kuonekana.”
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!