KIUNGO, Juan Mata amekataa kuvaa jezi namba 7 mgongoni katika
klabu ya Manchester United kabla ya jana Jumatatu kutambulisha jezi yake
mpya yenye namba 8 ambayo atakuwa akivaa.
Awali ilitarajiwa Mhispaniola huyo kuvaa jezi
namba 7 yenye hadhi kubwa Old Trafford, kwani iliwahi kuvaliwa na
wachezaji mahiri, Cristiano Ronaldo, David Beckham, George Best na Eric
Cantona.
Lakini, Mata aliyetua Man United kwa ada ya
uhamisho wa Pauni 37.1 milioni atavaa jezi namba 8 iliyokuwa ikitumiwa
na Mbrazili Anderson, ambaye amepelekwa Fiorentina kwa mkopo.
Kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter tayari
kumeibuka uvumi kwamba jezi hiyo namba 7 imeachwa wazi kwa ajili ya
Cristiano Ronaldo anayehusishwa na mpango wa kurejea Old Trafford kwenye
usajili wa Julai mwaka hu
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!