STRAIKA, Samuel Eto’o ametajwa kuwa ndiye mchezaji tajiri namba
moja kwenye Ligi Kuu England kwa wachezaji wa kigeni kwa kipato cha Dola
64 Milioni, imeelezwa.
Nafasi ya pili inashikwa na mkongwe wa Manchester
United, Ryan Giggs mwenye utajiri wa Dola 45 Milioni na Fernando Torres
yupo namba tatu kwa kuwa na Dola 42 Milioni.
Yaya Toure anashika namba nne na utajiri wake wa
Dola 41 Milioni, wakati staa wa Argentina, Sergio Aguero anakamilisha
tano bora na Dola zake 39 Milioni.
Ingawa ripoti zinadai kwamba Ligi Kuu England
imetawaliwa na wachezaji wa kigeni, kwenye orodha ya jumla ya 10 bora ya
matajiri kwa wachezaji wazawa inaongozwa na Wayne Rooney mwenye Dola 73
Milioni ikiwa ni zaidi ya Dola 20 Milioni kwa utajiri wa jumla wa
wachezaji wa kigeni.
Eto’o, 32, alitua Chelsea mwaka jana na kuonyesha
jeuri ya pesa baada ya kununua magari manne ya kifahari, Bugatti Veyron,
Aston Martin na Maybach Xenatec yaliyomgharimu Pauni 4 Milioni.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!