Serikali ya Sudan Kusini imewatuhumu waasi wa nchi hiyo kuwa
wamefanya ukatili dhidi ya raia kwa kuwaua wagonjwa 127 katika hospitali
ya mji wa Bor mwezi uliopita.
Maafisa wa serikali wanasema kuwa, mauaji hayo yalitokea Disemba 19 wakati kamanda Peter Gadet wa mji wa Bor alipokula kiapo cha utiifu kwa kiongozi wa waasi Riek Machar.
Ateny Wek Ateny msemaji wa Rais wa Sudan Kusini ameeleza kuwa, askari waasi walikwenda hospitalini na kuwachinja wagonjwa 127, madai ambayo yamekanusha na waasi hao. Badala yake waasi wa Sudan Kusini wamevituhumu vikosi vya serikali kuwa vimeua raia katika mji mkuu Juba na kuzorotesha uzalishaji wa mafuta katika mji wa Bentiu baada ya kuukomboa kutoka kwa waasi.
Wakati huo huo serikali ya Uganda imethibitisha kuwa askari wake 9 wameuawa nchini Sudan Kusini na wengine 12 kujeruhiwa.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!