Zaidi ya wapiganaji 40 kutoka makundi mbali mbali ya waasi huko
mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamejisalimisha kwa
Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO.
Kanali Felix Basse anayesimamia kituo cha MONUSCO amesema waasi hao
wamejisalimisha katika kipindi cha wiki moja iliyopita.
Ameongeza kuwa waasi waliojisalimisha ni kutoka makundi ya FDLR, Mai-Mai, UPCP, FPC pamoja na Mai-Mai-Nziza. MONUSCO imeanzisha oparesheni za kuangamiza waasi katika mkoa wa Kivu Kaskazini ambao unakumbwa na uasi. Kwingineko jana Martin Kobler Mkuu wa vikosi vya Umoja wa Mataifa nchini Kongo MONUSCO alisema kuwa, hali ya kibinadamu inayolikumba hivi sasa jimbo la Katanga kusini mashariki mwa Kongo, itabadilika na kuwa janga la kibinadamu. Kobler aliongeza kuwa, operesheni za kijeshi za vikosi vya Umoja wa Mataifa zimejikita zaidi katika majimbo ya Kivu na havipasi kughafilika na hali iliyoko katika jimbo la Katanga.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!