Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » KAMA WEWE MJANJA BASI SOMA HISTORIA HIZI ZINAZO AMBATANA NA SIKU KAMA YA LEO MYAKA KADHAA ILIYO PITA?

KAMA WEWE MJANJA BASI SOMA HISTORIA HIZI ZINAZO AMBATANA NA SIKU KAMA YA LEO MYAKA KADHAA ILIYO PITA?

Written By Unknown on Thursday, 30 January 2014 | Thursday, January 30, 2014

Siku kama ya leo miaka 80 iliyopita kipindi cha uongozi wa Adolph Hitler dikteta mbaguzi wa Kinazi wa Ujerumani kilianza. Chama cha Taifa cha Kisoshalisti cha Wafanyakazi wa Ujerumani ambacho kiliasisiwa na Hitler kilishinda viti 107 vya bunge katika uchaguzi wa mwaka 1930. Adolph Hitler alijitangaza kuwa kiongozi wa Ujerumani mwaka 1934 baada ya kuwa Kansela wa Ujerumani na Rais wa nchi hiyo. Hitler aliwafanya mamilioni ya wanadamu kuwa wahanga wa malengo yake ya kibaguzi. Hatua ya Adolph Hitler ya kuivamia Poland mwezi Septemba mwaka 1939 ilichochea Vita vya Pili vya Dunia ambapo hatimaye Ujerumani ilishindwa katika vita hivyo. Hitler alijiuwa mwaka 1945 baada ya Ujerumani kushindwa katika vita hivyo.
Miaka 66 iliyopita katika siku inayosadifiana na hii ya leo Mohandas Karamchand Gandhi, aliuawa kiongozi wa taifa na wananchi wa India na mpigania uhuru wa nchi hiyo. Gandhi alizaliwa mwaka 1869 na baada ya kukamilisha masomo alitunukiwa shahada ya digrii katika taaluma ya sheria nchini Uingereza. Mohandas Gandhi kwa muda fulani pia alikuwa kiongozi wa Wahindi wanamapambano huko Afrika Kusini. Gandhi pia aliwaongoza wananchi wanamapambano wa India dhidi ya serikali ya kikoloni ya Uingereza katika kupigania ukombozi wa nchi hiyo. India ilipata uhuru mwaka 1947 chini ya uongozi wa Gandhi.
Ma siku kama ya leo miaka 35 iliyopita mwafaka na tarehe 10 mwezi Bahman mwaka 1357 Hijria Shamsiya, wahadhiri na matabaka mengine ya wananchi walitangaza mshikamamo wao na kuamua kuungana na viongozi wa kidini waliokuwa wamekusanyika katika msikiti wa Chuo Kikuu cha Tehran nchini Iran kupinga utawala wa Shah. Idadi kubwa ya wananchi iliungana na wanazuoni hao katika Chuo Kikuu cha Tehran na hatimaye Shapour Bakhtiyar, Waziri Mkuu kibaraka wa utawala wa Shah akalazimika kukubali Imam Khomeini arejee nchini Iran kutoka uhamishoni nchini Ufaransa. Sambamba na hayo ndege za kijeshi za Marekani zilianza kuwaondoa raia wa nchi hiyo nchini Iran.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi