Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imepuuzilia mbali matamshi ya Rais
Barack Obama wa Marekani kuhusu Iran na kusema ‘hayasaidii chochote na
hayazingatii uhalisi wa mambo.’ Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya
Iran Marzieh Afkham amesema Jumatano kuwa matamshi ya Obama kuhusu
shughuli za nyuklia za Iran ni ishara ya ufahamu wake potofu kuhusu
kufungamana Tehran na shughuli za nyuklia zenye malengo ya amani.
Ameongeza kuwa, Marekani ina dhana potofu kuwa vikwazo ndivyo vilivyoipelekea Iran ikae kwenye meza ya mazungumzo ya nyuklia. Afkham alikuwa akiashiria hotuba ya kila mwaka ya Rais wa Marekani aliyotoa mbele ya Bunge la Kongresi la nchi hiyo Jumanne usiku. Afkham amekanusha madai ya Marekani kuwa miradi ya nyuklia ya Iran ina malengo ya kijeshi huku akisisitiza kuwa Tehran kamwe haijawahi kuwa na nia ya kumiliki silaha za nyuklia. Afkham amesema Iran inafungamana na mapatano ya awali ya nyuklia yaliyotiwa saini kati yake na madola sita makubwa duniani huko Geneva Novemba mwaka 2013. Ameitaka Marekani isisahau majukumu yake katika mkataba huo. Afkham pia amemkosoa Obama kwa kuitaja harakati ya Hizbullah ya Lebanon kuwa eti ni kundi la kigaidi. Amesema Marekani inatoa madai hayo huku ikifumbia jicho jinai za magaidi wa kitakfiri katika eneo.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!