Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » SOMA HISTORIA YA SIKU KAMA YA LEO MYAKA KADHAA ILIYO PITA HUKOO

SOMA HISTORIA YA SIKU KAMA YA LEO MYAKA KADHAA ILIYO PITA HUKOO

Written By Unknown on Thursday, 16 January 2014 | Thursday, January 16, 2014

Siku kama ya leo miaka 35 iliyopita Muhammad Reza Pahlavi mfalme wa mwisho wa Iran alikimbia nchi kwa kisingizio cha matibabu baada ya kupamba moto mapambano ya wananchi Waislamu wa Iran. Mwaka 1320 Hijria Shamsiya Muhammad Reza Pahlavi alikalia kiti cha usultani baada ya serikali ya Uingereza kumbaidisha baba yake, Reza Shah kutokana na hatua yake ya kuiunga mkono Ujerumani wakati wa Vita vya Pili vya Dunia. Mwaka 1332 Hijria Shamsiya Shah kwa mara nyingine tena aliikimbia Iran kufuatia mapambano ya wananchi, hata hivyo siku tatu baadaye yaani tarehe 28 mwezi Mordad, Shah alirejea nchini baada ya mapinduzi yaliyoendeshwa na Marekani na Uingereza dhidi ya wananchi wa Iran.
Miaka 168 iliyopita katika siku inayosadifiana na ya leo vita kati ya Marekani na Mexico vilianza kufuatia uvamizi uliofanywa na Marekani dhidi ya nchi hiyo. Marekani ilianzisha vita hivyo vilivyodumu kwa miaka miwili dhidi ya Mexico kwa kisingizio kwamba wahamiaji wa Marekani walikuwa wakisumbuliwa huko Mexico, lakini ukweli ni kuwa Marekani ilikuwa ikikusudia kuyaunganisha baadhi ya maeneo ya Mexico na ardhi yake khususan jimbo la Texas.
Na siku kama ya leo miaka 1371 iliyopita Yazid bin Muawiyya aliangamia. Yazid alikuwa mtawala dhalimu na fasiki na alitawala kwa muda wa miaka mitatu na miezi tisa. Katika kipindi cha utawala wake Yazid mwana wa Muawiyya alifanya kila aina ya jinai na alitambulika kwa ufuska. Miongoni mwa jinai zake ni kumuua shahidi mjukuu wa Mtume Muhammad SAW yaani Imam Hussein bin Ali AS na masahaba zake katika ardhi ya Karbala huko Iraq mwaka 61 Hijria, kushambulia kinyama miji mitakatifu ya Makka na Madina na kubomoa nyumba ya Mwenyezi Mungu yaani Al-Kaaba.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi