Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » HIYI NDO SABABU YA KUKWAMISHA KWA MAZUNGUMZO YA AMANI YA NCHINI SUDAN KUSINI

HIYI NDO SABABU YA KUKWAMISHA KWA MAZUNGUMZO YA AMANI YA NCHINI SUDAN KUSINI

Written By Unknown on Thursday, 16 January 2014 | Thursday, January 16, 2014

Taarifa zinasema kuwa mazungumzo ya kusaka amani kati ya pande hasimu za Sudan Kusini yanakwamishwa na hatua ya serikali ya Juba ya kukataa takwa la kuachiliwa huru wafungwa wa kisiasa.
Mabior Garang msemaji wa ujumbe wa waasi ulioko Addis Ababa Ethiopia amesema kuwa, haijaelezwa wafungwa hao vipi wataachiliwa huru na jambo hilo ndilo ajenda kuu ya mazungumzo. Ameongeza kuwa, ana wasiwasi upande wa serikali unatumia kadhia hiyo ya wafungwa kukwamisha mazungumzo ili uweze kujipatia ushindi kwenye medani ya vita.
Msemaji wa ujumbe wa serikali ya Sudan Kusini Michael Makuei amesema, serikali ya Juba haijakataa takwa hilo lakini imezigawa ajenda katika sehemu mbili, na hivi sasa wanajadili jinsi ya kumaliza uhasama na baadaye watajadili kadhia ya wafungwa.
Katika upande mwingine askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wamefyatua risasi na kuwatawanya wapiganaji waliokuwa karibu na kituo cha umoja huo cha Malakal, baada ya watu waliokuwa na silaha kuingia kwenye kituo hicho ambapo makumi ya wakimbizi walijeruhiwa na mmoja kuuawa.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi