Rais wa muda wa Jamhuri ya Afrika ya Kati amesema yuko tayari
kufanya mazungumzo ya makundi ya wanamgambo wanaobeba silaha nchini
humo.
Catherine Samba-Panza aliwaambia waandishi habari jana mjini Bangui kuwa lengo la mazungumzo kama hayo ni kukomesha machafuko ya sasa na kurejesha amani na utulivu nchini humo. Alisema sababu zilizoyafanya makundi ya wanamgambo kushika silaha zinapaswa kupewa mazingatio na kutafutiwa ufumbuzi.
Catherine Samba-Panza ambaye alikuwa meya wa jiji la Bangui alichaguliwa siku chache zilizopita kuwa Rais wa muda wa Jamhuri ya Afrika ya Kati. kiongozi huyo anakabiliwa na changamoto kadhaa kubwa ikiwa ni pamoja na kudhibiti makundi ya wanamgambo wanaobeba silaha kama Anti Balaka na Seleka, kurejesha amani nchini kote hususan katika mji mkuu Bangui na kuanzisha upya shughuli za taasisi mbalimbali za serikali.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!