Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » HATIMAYE PENTAGON NA NSA ZAMPANGIA NJAMA ZAKUMUUWA SNOWDEN

HATIMAYE PENTAGON NA NSA ZAMPANGIA NJAMA ZAKUMUUWA SNOWDEN

Written By Unknown on Wednesday, 22 January 2014 | Wednesday, January 22, 2014

Wakili wa Edward Snowden, mfanyakazi wa zamani wa vyombo vya ujasusi vya Marekani aliyekimbilia nje ya nchi, amesema kuwa mteja wake anahofia kuuawa baada ya vitisho vilivyotolewa na maafisa wa serikali ya Washington.
Anatoly Kucherena amesema kuwa maisha ya Edward Snowden yamo hatarini na amewataka viongozi wa serikali ya Washington kuchunguza vitisho vilivyotolewa dhidi ya mteja wake. Amesema afisa wa Wakala wa Usalama wa Taifa wa Marekani (NSA) aliyetoa amri ya kuuliwa Snowden anapaswa kutambuliwa na kujulikana.
Edward Snowden ambaye alikuwa mfanyakazi wa mashirika ya ujisasu ya Marekani alituhumiwa na serikali ya Washington kwa kufichua siri za ujasusi wa nchi hiyo nje ya nchi na akatoroka nchi. Kwa sasa jasusi huyo wa zamani wa Marekani amepewa hifadhi nchini Russia.
Siku chache zilizopita kituo kimoja cha habari kilifichua kuwa afisa mmoja wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) na mwingine wa NSA wanapanga mikakati ya kumuua jajusi huyo wa zamani wa Marekani anayesakwa kwa udi na uvumba.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi