RAIS wa Barcelona, Sandro Rosell ameachia ngazi na kuwalaumu
wale wote wanaomshambulia kutokana na kashfa ya pesa katika uhamisho wa
staa wa timu hiyo, Neymar kutoka klabu yake ya zamani, Santos.
Rosell na Barcelona kwa sasa wanachunguzwa na
Mahakama Kuu Hispania kutokana na kashfa ya hesabu mbovu za pesa katika
uhamisho huo wa Neymar uliofanyika kipindi cha majira ya joto.
Mabingwa hao wa Hispania walimnunua Neymar kwa
kiasi cha Euro 57 milioni Mei mwaka jana, lakini inasemekana ni kiasi
cha Euro 17 milioni tu ndizo zilizoingia katika akaunti ya Santos.
“Mimi na familia yangu kwa muda mrefu sasa
tumeumia na mashambulizi haya ambayo yamenifanya nijiulize kama ina
maana yoyote kuwa rais. Katika siku za karibuni kumekuwa na shutuma
zisizo na maana kwangu kutoka mahakamani. Nasisitiza kwamba kila kitu
kilikwenda sawa katika uhamisho wa Neymar,” alisema Rosell.
Majaji nchini Hispania wamekubali kuanza kusikiliza kesi ya uhamisho wa staa huyo baada ya kugundulika kuwa wa kiujanjaujanja.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!