Katika siku kama ya leo miaka 558 iliyopita, iliyopita kazi ya
uchapishaji vitabu ilianza na kitabu cha kwanza kabisa kikachapishwa kwa
kutumia mashine iliyogunduliwa na Mjerumani Johannes Gutenberg. Mashine
hiyo ya uchapishaji ilikuwa hatua muhimu katika njia ya uchapishaji na
uenezaji wa elimu na maarifa kati ya wanadamu. Katika zama zake,
Johannes Gutenberg pia alichapisha kitabu cha Biblia maarufu kwa jina
la' Gutenberg Bible.' Hii leo kurasa kadhaa zilizobakia za kitabu hicho
zinahifadhiwa katika jumba la makumbusho.
***
Siku kama ya jana miaka 143 iliyopita vijidudu maradhi
vinavyosababisha maradhi ya ukoma viligunduliwa na tabibu na mhakiki wa
Norway kwa jina la Gerhard Henrik Armauer Hansen. Ugonjwa huo huambatana
na vidonda vikali vinavyovuruga na kuharibu maumbo ya muathirika.
Vijidudu maradhi vya ugonjwa huo wa ukoma pia hukusanyika katika mishipa
ya neva na kusababisha uharibifu katika sehemu kubwa ya mishipa ya
neva. Maradhi hayo hujitokeza zaidi katika maeneo yenye joto. Licha ya
maendeleo makubwa ya kisayansi yaliyopatikana katika kudhibiti ugonjwa
wa ukoma, lakini njia ya kutibu maradhi hayo sugu bado haijapatikana na
kuna idadi kubwa ya waathirika wake wanaendelea kuteseka katika nchi
mbalimbali duniani.
***
Siku kama ya jana miaka 7 iliyopita Harakati ya Mapambano ya Kiislamu
ya Palestina HAMAS ilipata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa Bunge
ikiwa ni mara ya kwanza kwa harakati hiyo kushiriki kwenye zoezi hilo.
Katika uchaguzi huo uliosimamiwa na waangalizi wa kigeni, Hamas
ilifanikiwa kupata viti 76 kati ya jumla viti 132 vya Bunge la Palestina
licha ya propaganda chafu zilizokuwa zikifanywa na vyombo vya habari
vya nchi za Magharibi. Kwa utaratibu huo Hamas ilimuarifisha Ismail
Hania kama Waziri Mkuu na kutangaza kwamba itaunda serikali ya umoja wa
kitaifa. Hata hivyo nchi za Magharibi zikiongozwa na Marekani na
muitifaki wake Israel, zilikataa kutambua rasmi serikali hiyo
iliyochaguliwa kidemokrasia na wananchi wa Palestina.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!