Umoja wa Mataifa (UN) umetangaza kuwa una wasiwasi kuhusu juhudi
zinazofanywa na jeshi la Sudan Kusini za kutaka kuvamia kambi ya
wakimbizi wa machafuko na vita vinavyoendelea nchini humo.
Kituo cha habari cha al Masri al Youm kimeripoti leo kuwa msemaji wa Umoja wa Mataifa Martin Nesirky akisema kuwa baada ya kudhibiti mji wa Bor askari wa serikali ya Sudan Kusini wanafanya jitihada za kuvamia kambi ya wakimbizi iliyoko chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa. Nesirky amesema uvamizi huo unaweza kusababisha maafa kwa wakimbizi walioko kwenye kambi hiyo.
Msemaji wa Umoja wa Mataifa ameongeza kuwa kambi za wakimbizi zinapaswa kuepushwa na mapigano na vitendo vya ukatili na kwamba viongozi wa kijeshi na hata wa serikali ya Sudan Kusini hawapaswi kuingia katika kambi hizo.
Sudan Kusini imetumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya jeshi la serikali ya Juba na askari waasi wanaoongozwa na makamu wa zamani wa rais wa nchi hiyo Riek Machar. Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa watu elfu kumi wameuawa katika mapigano hayo yaliyoanza tarehe 15 Disemba mwaka uliopita.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!