Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ametangaza baraza
lake la mawaziri huku akiwahamisha na kuwateua mawaziri na Naibu
Mawaziri kuziba nafasi zilzioachwa wazi na wale waliojiuzulu. Baraza hilo
limekua likisubiriwa na idadi kubwa ya watanzania, lakini baahi ya
watanzania wamebaini kwamba uteuzi wa baadhi ya mawiziri
haukuwashangaza.
Kwenye uteuzi huo ambao ulikuwa unasubiriwa kwa hamu na gamu na
wananchi wa Tanzania, umeshuhudia mabadiliko machache kwenye baadhi ya
wizara huku wale waliolalamikiwa na wabunge wakiendelea kubakia kwenye
wizara zao.
Kwenye uteuzi wake rais Kikwete amemteua aliyekuwa naibu katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Dr Asha Rose Migiro kuwa waziri wa katiba na sheria, huku wizara ya ulinzi ambaye waziri wake alijiuzulu, ikichukuliwa na Dkt Hussein Mwinyi aliyekuwa wizara ya afya, wakati wizara ya Mambo ya ndani ikichukuliwa na Mathias Chikawe ambapo wizara ya maliasili na utalii ameteuliwa Lazaro Nyalandu aliyekuwa naibu waziri.
Baadhi ya wachambuzi wa mambo wanamtazamo chanya kuhusu bararaza hli jipya, wengine wakiwa hawana imani na baraza lenyewe.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!