Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu limeripoti kuwa
limegundua na kuzika maiti za watu 50 katika maeneo ya kaskazini
magharibi mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Taarifa iliyotolewa jana na Shirika la Msalaba Mwekundu ilisema kuwa maiti hizo za watu waliouawa zilipatikana katika maeneo ya Bossembele, Boyali na Boali.
Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati Georgios Georgantas amesema kuwa wakazi wa maeneo hayo hawana ulinzi wa aina yoyote na wanalazimika kukimbia makazi yao kwa hofu ya kushambuliwa na makundi ya wanamgambo wanaobeba silaha.
Jumuiya zisizo za serikali zinazofanya kazi katika maeneo hayo zinasema kuwa hali ya wakazi wa maeneo hayo ni mbaya sana na kwamba ni maafa yasiweza kudhibitiwa.
Maeneo mengi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati yangali yanashuhudiwa wimbi kubwa la mauaji yanayofanywa dhidi ya raia licha ya askari wa kulinda amani wa kimataifa kuimarisha usalama wa kiwango fulani katika mji mkuu wa nchi hiyo Bangui.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!