Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » VLADIMIR PUTIN RAIS WA RUSSIA AIPONGEZA SERIKALI YA IRAN KWA KUENDELEZA MAZUNGUMZO YA NYUKLIA

VLADIMIR PUTIN RAIS WA RUSSIA AIPONGEZA SERIKALI YA IRAN KWA KUENDELEZA MAZUNGUMZO YA NYUKLIA

Written By Unknown on Friday, 17 January 2014 | Friday, January 17, 2014

Rais Vladimir Putin wa Russia amepongeza juhudi za Iran katika kuendeleza mazungumzo ya nyuklia na nchi sita zenye nguvu duniani. Mazungumzo hayo yalipelekea kutiwa saini mkataba wa nyuklia wa Geneva mwaka jana.
Akizungumza Alkhamisi mjini Moscow wakati alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif, Putin alipongeza hatua zilizopigwa katika mazungumzo hayo kati ya Iran na madola sita makubwa duniani ambayo ni Russia, China, Marekani, Ufaransa, Uingereza na Ujerumani. Mazungumzo hayo yanalenga kutatua mgogoro ulioibuliwa na nchi za Magharibi kuhusu mpango wa Iran wa kuzalisha nishati ya nyuklia kwa malengo ya amani. Putin aidha ametaka kuwepo ushirikiano zaidi wa kiuchumi baina ya Tehran na Moscow. Rais wa Russia pia amesisitiza kuhusu msimamo wa nchi yake kuunga mkono kushiriki Iran katika kongamano lijalo la Geneva II kuhusu  Syria. Kongamano hilo linatazamiwa kuanza Januari 22 katika mji wa Montreux Uswisi. Zarif kwa upande wake ameishukuru Russia kwa mchango waka katika utatuzi wa kadhia ya nyuklia ya Iran.  Katika kikao hicho Rais Putin alitangaza kukubali mwaliko wa Rais Hassan Rouhani wa kuitembelea Iran.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi