Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » KAMA ULIKUWA HUFAHAMU BASI,SOMA HISTORIA YA SIKU KAMA YA LEO MYAKA KADHAA ILIYO PITA

KAMA ULIKUWA HUFAHAMU BASI,SOMA HISTORIA YA SIKU KAMA YA LEO MYAKA KADHAA ILIYO PITA

Written By Unknown on Friday, 17 January 2014 | Friday, January 17, 2014


Siku kama ya leo miaka 5
iliyopita Wazayuni maghasibu walilazimika kutangaza usitishaji vita baada ya jeshi la utawala wa Israel kufanya mashambulizi ya kinyama ya siku 22 dhidi ya raia wa Ukanda wa Ghaza. Katika mashambulizi hayo, utawala wa Kizayuni ulikusudia kuiangamiza Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas au kwa uchache kuilazimisha harakati hiyo ikubali mazungumzo eti ya mapatano. Hata hivyo uungaji mkono wa Wapalestina kwa harakati ya Hamas na vilevile malalamiko makali ya walimwengu dhidi ya jinai za wanajeshi wa Israel katika Ukanda wa Ghaza, uliulazimisha utawala haramu wa Israel usitishe mashambulio yake.
Miaka 58 iliyopita, siku kama ya leo ya tarehe 27 Dey 1334 Hijria Shamsia, Nawwab Safavi, mwanachuoni na mwanaharakati wa Iran aliuawa shahidi pamoja na wenzake watatu, baada ya kuhukumiwa adhabu ya kifo kwenye mahakama ya kimaonyesho tu ya kijeshi katika utawala wa Shah nchini  Iran. Akiwa kijana, Nawwab Safavi alipata taaluma ya masomo ya kidini nchini Iran na kisha akaelekea Najaf nchini Iraq kwa shabaha ya kujipatia elimu zaidi. Alirejea nchini humo baada ya miaka kadhaa na kuanzisha mapambano dhidi ya utawala tegemezi na kibaraka wa Shah. Hatimaye katika siku kama hii ya leo Safavi alitawa na utawala wa Shah na kuuawa shahidi akiwa na wenzake watatu.
Na miaka 173 iliyopita mlima mrefu zaidi duniani uligunduliwa na mpanda milima wa Kiingereza kwa jina la George Everest na mlima huo ukapewa jina lake. Hata hivyo, George Everest alishindwa kufika juu ya kilele cha mlima huo. Wapanda milima wawili kutoka India na Uingereza walifanikiwa kufika juu ya kilele cha mlima huo mwaka 1953.
Mlima Everest una urefu wa mita 8800 na ni katika silsila ya milima ya Himalaya ambayo inaanzia kaskazini mwa India hadi magharibi mwa Uchina.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi