Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » BADO NCHI YA MAREKANI YAENDELEA KUUINGIZA KWA NGUVU UTAMADUNI WA MAGHARIBI BARANI AFRICA

BADO NCHI YA MAREKANI YAENDELEA KUUINGIZA KWA NGUVU UTAMADUNI WA MAGHARIBI BARANI AFRICA

Written By Unknown on Monday, 17 February 2014 | Monday, February 17, 2014

Katika fremu ya sera za Ikulu ya Marekani White House za kueneza utamaduni na mtindo wa maisha wa Kimagharibi katika nchi za Kiafrika, Rais Barack Obama wa Marekani amepinga vikali mchakato wa kupasisha sheria inayopiga marufuku usenge na usagaji nchini Uganda.
Rais wa Marekani ambaye jana alijionesha kama mtetezi wa haki za binadamu, alisema kuwa juhudi za Rais Yoweri Museveni wa Uganda za kutaka kupasisha sheria inayopiga marufuku maingiliano ya kujamiiana kati ya watu wenye jinsia moja zitatatiza uhusiano wa nchi hizo mbili. Obama amemtaja Museveni kuwa ni hatari kwa watu wanaojamiiana kinyume na maumbile nchini Uganda na ameituhumu nchi hiyo kuwa haiheshimu haki za binadamu!
Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda Jumamosi iliyopita alisisitiza kuwa anaunga mkono muswada uliopasishwa na Bunge la Uganda unaotambua maingiliano kinyume na maumbile kuwa ni kosa la jinai na kupiga marufuku vitendo hivyo nchini Uganda. Museveni pia amesema yuko tayari kuingia vitani na makundi ya kigeni yanayowatetea mabaradhuli.
Waafrika wanapinga vikali vitendo vya kujamiiana kinyume na maumbile na na wanasisitiza juu ya kushikamana na thamani za asili na kidini. Hivi karibuni pia Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria alipasisha sheria inayopiga marufuku ndoa kati ya watu wenye jinsia moja nchini humo na kusema kuwa vitendo hivyo vichafu haviwiani na mitazamo na itikadi za Waafrika.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi