Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » WACHAMBUZI WANASEMA KUWA TIMU YA BAYERN MUNICH IMEKAMILIKA KUZIDI HATA BARCELONA,NA HAITASHANGAZI HAWA KUNYAKUWA KOMBE LA UEFA

WACHAMBUZI WANASEMA KUWA TIMU YA BAYERN MUNICH IMEKAMILIKA KUZIDI HATA BARCELONA,NA HAITASHANGAZI HAWA KUNYAKUWA KOMBE LA UEFA

Written By Unknown on Tuesday, 18 February 2014 | Tuesday, February 18, 2014

Miaka 22 tangu kubadilishwa kwa jina na mfumo - hakuna timu ambayo imeweza kutetea taji la ligi ya mabingwa wa ulaya. Baadhi ya washindi walikaribia kufanya hivyo - timu nne zikipoteza kwenye fainali na sita katika nusu fainali - lakini kikosi cha Arrigo Sacchi cha AC Milan kinabakia kuwa ndio timu pekee kuwahi kutetea ubingwa wa ulaya miaka 24 iliyopita.

Mwiko huu umekuwa ukipata umaarufu kila mwaka kwa sababu mabingwa watetezi wamekuwa wakishindwa kutetea kombe lao.

Olympique de Marseille walishindwa kutetea ubingwa wao wa mwaka 1993 kufuatia skendo ya rushwa ya Valenciennes, Porto iliuza wachezaji wao muhimu waliochukua ubingwa wa 2004, wakati Borussia Dortmund '97, AC Milan 2007, Inter 2010 na Chelsea 2012 walishindwa kutokana na kuwa vikosi vilivyokuwa na wachezaji wenye umri mkubwa na vilihitaji kujengwa upya.

Timu ambazo zilikuwa na nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wa Champions League zilikuwa Ajax ya Luis van Gaal ya mwaka 1996, kikosi cha Marcello Lippi cha Juventus mwaka mmoja uliofuatia, Vicente Del Bosque na Real Madrid mwaka 2003, miaka iliyofuatia Milan chini ya Carlo Ancelotti na Pep Guardiola na Barcelona mwaka 2010. Kikosi cha Fabio Capello cha Milan cha 1995 na Sir Alex Ferguson na Manchester United ya 2009 - timu hizi zingeweza kutetea ubingwa wao lakini walishindwa kuvunja mwiko wa kutetea ubingwa wa Champions League.

Hata hivyo, ukiangalia vigezo na uwezo - hakuna timu katika vilabu vyote vilivyotajwa hapo juu ambayo ilikuwa nafasi nzuri ya kutetea ubingwa kama ambavyo ilivyo kwa Bayern Munich msimu huu.



NAMBA
Bayern in 2013-14
99Namba ya mabao Bayern wamefunga msimu huu katika jumla ya mechi 35. 
30Namba ya mechi za ushindi - wameshindwa kushinda katika mechi 5, moja kati hizo mechi walishinda kwenye mikwaju ya penati.
21Clean sheets ambazo magolikipa  Manuel Neuer na Tom Starke msimu huu.
16Namba ya pointi ambazo Bayern imeizid timu inayoshika nafsi ya pili Bundesiliga. 
13Mechi ambazo Beyern wameshinda mfululizo msimu huu.
0Namba ya mechi ambazo wamepoteza msimu huu kwenye Bundesliga

Tangu mwanzoni mwa 2013, Bayern wamecheza jumla ya mechi 62. Wameshinda 55, wakitoa sare 4 na kupoteza mara 3 tu - mechi mbili kati ya 3 walizofungwa zilikuwa za Champions league lakini waliweza kufuzu na kuendelea mbele. Wamefunga mabao 179 na kuwa na clean sheets 36. Bayern wapo kwenye mfululizo wa kushinda 13 za Bundesiliga - hawajafungwa katika ligi katika kwa miezi 16 sasa na wamebeba makombe matano kutoka msimu uliopita.

Takwimu ni za kuvutia mno, kwa mchezaji mmoja mmoja, timu nzima, kiufundi, kimbinu, kiakili, kimwili - Bayern ni timu iliyokamilika. Kuna ubora mkubwa kwenye kila eneo - golikipa Manuel Neuer, walinzi David Alaba na Dante, viungo Philipp Lahm, Bastian Schweinsteiger na Thiago, washambuliaji Franck Ribery, Arjen Robben na Thomas Muller – listi inaendelea. Na bila kumsahau kocha Pep Guardiola, ambaye ana rekdoi nzuri mno kwenye michuano hii - makombe mawili na nusu fainali mbili katika miaka minne aliyokaa Barcelona. 



Bayern inaweza isiwe timu bora kabisa katika zama hizi za Champions League, lakini haijawahi kutokea kwa timu nyingine kuwa na ubora mkubwa tofauti na wapinzani wake kama ilivyo sasa. Huko nyuma miaka ya tisini katikati Ajax walikuwa na upinzani kutoka kwa Juve iliyokuwa vizuri mno - ambao walienda kucheza fainali mara 3. Waitaliano hao pia walikumbana na upinzani kutoka kwenye vikosi bora vya Dortmund iliyokuwa na magwiji wa kijerumani na  Manchester United ya 99.
Magalatico wa Real Madrid -  Zinedine Zidane, Luis Figo, Raul na Ronaldo De Lima walikuwa na bahari mbaya ya kushiriki katika msimu mgumu kabisa wa Champions League msimu wa 2002-03. Waliocheza fainali waitaliano Juve vs AC milan walikuwa bora zaidi, wakati Inter na Valencia pia walikuwa sawa. Wakati kikosi cha Ancelotti kiliposhindwa kutetea ubingwa msimu uliofuatia - vilikuwepo vikosi vikali kama Arsenal 'wasiofungika' na watoto wa Mourinho chini ya umiliki mpya Roman Abramovich.
Kikosi cha Guardiola cha mwaka  2010 – wakiwa na staili yao nzuri ya tiki-taka na mastaa kama Lionel Messi, Andres Iniesta na Xavi - walionekana wangeweza kuuvunja mwiko huo, lakini ilisahaulika namna Inter Milan walivyo na rekodi nzuri kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano hii. Kikosi cha Jose Mourinho kilichochukua makombe matatu kilikuwa na safu nzuri ya ulinzi kuliko zote barani ulaya, iliyokuwa ikiongozwa na Lucio na Walter Samuel. 



Vikosi vinavyoshindana na Bayern msimu huu kwenye karatasi wanaonekana hawana viwango ambavyo wapinzani wa mabingwa wa zamani walivyokuwa navyo. Barcelona wanaonekana wapo kwenye anguko, Atletico hawana uzoefu mzuri, Manchester United ndio wabovu kabisa, Arsenal wanaonekana kuchoka na wanahitaji miujiza kuweza kuvuka kwenda robo fainali. wakati huo huo Manchester City wana utegemezi mkubwa kwa wachezaji wao muhimu wachache. Real Madrid, PSG na Chelsea wanaokuja vizuri huwezi kuwatoa kwenye kinyang'anyiro, lakini Bayern wapo kwenye sayari nyingine.
Ubora wa kikosi chao cha kwanza mpaka cha pilini hatari. Pamoja na kuwa wanamkosa Bastian Schweinsteiger, Javi Martinez, Arjen Robben, Franck Ribery na Holger Badtsuber lakini Bayern wameweza kuwa katika kiwango bora msimu huu wakivunja rekodi kadhaa. Guardiola ana kikosi kizuri kiasi kwamba ameweza hata kuwatupa nje ya kikosi Toni Kroos na Mario Mandzukic. Ukikitoa kikosic ha Milan chini ya Capello - hakuna kikosi cha timu inayoshiriki Champions league kilichokuwa na utajiri wa wachezaji kiasi cha kuweza kumudu hali ya kuondokewa na wachezaji na wachezaji muhimu zaidi ya 7 ndani ya msimu mmoja.
Na huku wakiwa na pointi 16 zaidi kileleni mwa Bundesliga, Guardiola anaweza kuendelea kukizungusha kikosi chake na kuhakikisha wanakuwa na nguvu ya ziada kwa ajili ya kumalizia biashara ya Champions League. Mpaka kufikia mwishoni mwa mwezi ujao Bayern wanaweza kuwa tayari wameshatetea ubingwa wao. Mbio za ubingwa wa premier league na La Liga zinazidi kuwa ngumu, timu kadhaa zikigombea ubingwa huo. Kuanzia March, Aprill na May - watakuwa na nguvu mpya kwa sababu kuna mapumziko ya kipindi cha baridi katika ligi ya Ujerumani. Ni mabingwa wachache waliopita wa UCL waliowahi kuwa na faida hii.
Pamoja na ubora walionao lakini vilevile Bayern wana njaa ya kufanikiwa tena. Huku wakiwa na kocha mpya Guardiola, mfumo mpya, hakuna ambaye ana uhakika wa namba katika kikosi cha mhispania huyo, hivyo hakuna nafasi ya mchezaji kutokujituma na kufanya ujinga. Hii haijawahi kutokea huko nyuma - kikosi cha Ancelotti kiliongoza kwa mabao 4-1 katika mechi ya kwanza cha mchezo wa nusu fainali dhidi ya Deportivo lakini wakata mguu wao kwenye gia ya mafuta, matokeo wakatandikwa 4-0 katika mchezo wa pili na kuaga mashindano.

"Mabadiliko ya kocha ndani ya timu yamewafanya kutoacha kujituma zaidi, pia uwepo wa michuano ya kombe la dunia. Kila mtu anacheza kwa kujituma kwa asilimia 10 katika kila mechi. Wachezaji wana njaa mbaya. Wanataka kufanya kitu ambacho hakuna mwingine amewahi kufanya hivyo. Hiki kitu kinawasukuma kucheza vizuri zaidi," alisema nahodha wa zamani wa timu hiyo Stefan Effenberg.


Ama kwa hakika kikosi hiki cha Bayern kinaweza kutengeneza historia mpya. Ikiwa watashindwa, basi itabidi tukubaliane kwamba mwiko wa kutetea ubingwa wa Champions league utabaki milele.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi