KINDA Adnan Januzaj amepigiwa simu na Naibu Waziri Mkuu wa Kosovo kuombwa aichezee mechi ya kwanza ya kimataifa nchi hiyo.
![]()  | 
| Tishio jipya: Januzaj alianza kutisha katika Ligi Kuu ya England mapema msimu huu kwa kufunga mabao yote mawili katika ushindi wa 2-1 wa United dhidi ya Sunderland | 
Behgjet
 Pacolli, bilionea mmiliki kampuni za ujenzi anayekadiriwa kuwa na 
utajiri wa Dola za Kimarekani Milioni 550, anajaribu kumshawishi Januzaj
 acheze dhidi ya Haiti mwezi ujao.
Januzaj,
 mwenye umri wa miaka 19, badohajaamua acheze nchi gani soka ya 
kimataifa, lakini familia yake ilikuwa moja ya wanaharakati wa uhuru wa 
nchi hiyo.
![]()  | 
| Wito Kosovo: Kosovo imemkaribisha mchezaji wa Manchester United, Adnan Januzaj aichezee timu yao ya taifa | 
Pamoja
 na hayo, Kosovo bado haijapata uanachama wa FIFA, wameruhusiwa kucheza 
mechi ya kwanza ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Haiti mwezi ujao.
Januzaj alizaliwa mjini Brussels, Ubelgiji lakini kuna utata mkubwa juu ya mustakabali wake katika soka ya kimataifa.
England ni moja ya nchi ambazo zinatumaini kumpata Januzaj.




0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!