WAPO
 njiani. Cesc Fabregas ameweka kwenye picha kwenye akaunti yake ya 
Instagram wakiwa kwenye ndege hiyo jana Jumatatu na wachezaji wenzake wa 
Barcelona kuelekea England kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi 
Manchester City.
![]()  | 
| Tayari kuondoka: Cesc Fabregas ameposti picha hii katika Instagram yake akiwa na Alex Song, Gerard Pique na Carles Puyol kwenye ndege kwa ajili ya mechi dhidi ya City kesho usiku | 
Ameposti
 picha akiwa na wachezaji wenzake Alex Song, Carles Puyol na Gerard 
Pique wakati ndege inataka kuruka mabingwa hao wa Hispania wakienda jiji
 la Manchester kwa ajili ya mechi ya kwanza ya hatua ya 16 Bora, 
itakayopigwa Uwanja wa Etihad hii leo usiku.
Wakiwa wamevalia suti za kimichezo nyekundu, wachezaji hao walionekana vizuri na walio tayari kwa mpambano huo mgumu wa ugenini.
Barcelona
 inakwenda kwenye mechi hiyo ikitoka kuichapa mabao 6-0 Rayo Vallecano 
Jumamosi katika La Liga, matokeo ambayo yanawafanya waendelee kukabana 
koo na Real Madrid na Atletico kileleni.
Lakini
 watakutana na Manchester City ambayo pia iko vizuri, ikiwa imetoka 
kuing'oa Chelsea katika Raundi ya Tano ya Kombe la FA mwishoni mwa wiki 
na kocha Manuel Pellegrini, ambaye ana uzoefu wa kucheza na Barca, anajiamini City inaweza kufanya vizuri katika mchezo huo.




0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!