![]()  | 
| Rio Ferdinand akila pozi na mzee Maradona pande za Dubai | 
WACHEZAJI
 wa Manchester United wamekutana na kuzungumza naye, gwji wa soka 
duniani, Diego Maradona katika kambi yao ya mazoezi nchini Dubai.
Kiungo
 huyo mstaafu wa Argentina, maarufu zaidi kwa 'Mkono wa Mungu' kutokana 
na kuifunga bao la mkono England katika Fainali za Kombe la Dunia mwaka 
1986, alikutana na nyota hao walioweka kambi ya wiki moja huko.
![]()  | 
| Mkali wa mabao: Mshambuliaji wa Uholanzi, Robin van Persie akiwa na Diego Maradona ambaye ni shujaa wake | 
Robin
 van Persie, Juan Mata, Rio Ferdinand na David de Gea walikuwa miongoni 
mwa wachezaji wa United waliopiga picha na mchezaji huyo mwenye umri wa 
miaka 53, ambazo waliziposti kwenye mitandao yao ya kijamii.
 
Maradona
 ni kipenzi cha wengi miongoni mwa wapenzi na wadau wa soka, wakiwemo 
wachezaji wenyewe na Mata na Van Persie wamesema wao ni mashabiki wa 
wakubwa wa gwiji huyo.
![]()  | 
| Kipa wa United, David de Gea akiwa na Maradona | 
Nyota
 hao wawili wa United walishindwa kuficha furaha yao baada ya kumuona 
Maradona akiwasili kwenye viwanja walivyokuwa wanafanya mazoezi na 
haraka wakaenda kuposti juu ya mchezaji huyo wa zamani wa Boca Juniors 
kwenye Twitter.
"Mabibi na mabwana, mtumia mguu wa kushoto bora daima! EL DIEGO. #Maradona," alisema Mata.
Van Persie alisema: "Babu kubwa kukutana na shujaa wangu tena, Diego bora daima,". 
![]()  | 
| Babu kubwa: Kiungo wa Hispania, Juan Mata hakukosa nafasi ya kupicha picha na Maradona | 
Maradona
 alikuwa hatari sana anapoingia kwenye eneo la mita 18 la wapinzani na 
haikuwa ajabu Ferdinand na de Gea walitumia fursa hiyo kupata ushauri 
kutoka kwa mkali huyo wa zamani wa Argentina.
Ferdinand
 aliposti picha akiwa na Maradona kwenye Instagram yake, akiambatanisha 
na maelezo: "Mimi na #Gwiji#DiegoMaradona #Mkuu".
Kipa De Gea ameandika: "Babu kubwa kuwa namba 10 bora!! "El Pelusa"'
Nyota
 huyo wa Amerika Kusini yupo kwa muda mrefu Dubai na amekuwa kocha wa Al
 Wasl FC inayoshiriki ya Ligi ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), hadi 
mwaka 2012.
United imefuata hali ya hewa ya joto Dubai ili kufanya mazoezi ya wiki moja.






0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!