Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » UKIWA UTAJIULIZA MENGI ILA MOJA TAMBUWA KUWA LULU AMEKIRI MBELE YA MAHAKAMA KUWA YEYE NA KANUMBA WALIKUWA WAPENZI,HUKU SWALA KUUWA BILA KUKUSUDIA AKILIKANA

UKIWA UTAJIULIZA MENGI ILA MOJA TAMBUWA KUWA LULU AMEKIRI MBELE YA MAHAKAMA KUWA YEYE NA KANUMBA WALIKUWA WAPENZI,HUKU SWALA KUUWA BILA KUKUSUDIA AKILIKANA

Written By Unknown on Tuesday, 18 February 2014 | Tuesday, February 18, 2014

Kesi ya kuua bila kukusudia inayomkabiri muigizaji wa kike kutoka nchini Tanzania, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu imesikilizwa jana (February 17) katika mahakama kuu, Kanda ya Dar es Salaam.
Lulu alikiri mbele ya Jaji Rose Temba kuwa alikuwa na uhusiano wa mapenzi na marehemu Steven Kanumba na kwamba walikuwa na ugomvi, lakini alikana mashitaka ya kumuua bila kukusudia.
Mbali na kukiri kuwa na uhusianano wa mapenzi, muigizaji huyo pia alikiri kuwa baada ya tukio hilo alitoka nje ya chumba walichokuwepo na kwenda kumwambia mdogo wake marehemu Kanumba, Setti Bosco kuwa Kanumba ametangulia mbele ya haki.
Kanumba na Lulu enzi hizo picha ya kwenye filamu ya Familly tears
Kaburi la Kanumba
Akisoma hati ya mashitaka, Wakili Mwandamizi wa Serikali, Monica Mbogo, alidai kuwa Aprili 7, mwaka 2012, Sinza Vatikani, Mkoa wa Dar es salaam nchini Tanzania, mshitakiwa alimuua bila kukusudia Steven Kanumba.
Wakili Kombo, alidai kuwa pamoja na mambo mengine, marehemu Kanumba baada ya kufa, mwili wake ulipelekwa hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo majibu yanaonyesha kwamba kifo chake kimesababishwa na uvimbe ndani ya ubongo.
Upande wa serikali una mashahidi watano pamoja na vielelezo wakati upande wa utetezi pia unatarajia kuwa na mashahidi watano na vielelezo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi