NAHODHA wa klabu ya
Manchester United Nemanja Vidic amebainisha kuwa anatarajia kuondoka
mwishoni mwa msimu huu. Beki huyo wa kimataifa wa Serbia ambaye mkataba
wake unaisha kiangazi, alianza kuitumikia United mwaka 2006. Vidic
aliiambia tovuti ya klabu hiyo kuwa hana mpango wowote wa kucheza katika
timu yoyote nchini Uingereza kwani timu pekee aliyokuwa akitaka
kuichezea ilikuwa Manchester United.
Nyota huyo amesema ni jambo ambalo
hakulitegemea kushinda mataji 15 akiwa hapo, hata hivyo ameamua kuondoka
msimu huu ili kutafuta changamoto mpya sehemu nyingine. Vidic ambaye
alinunuliwa kwa paundi milioni 7 kutoka klabu ya Spartak Moscow alitua
rasmi United katika siku ya Christmas mwaka 2005, alikuwa nahodha wakati
United ikishinda taji lake la 20 la Ligi Kuu huku kwa upande wake
ilikiwa la tano chini ya Sir Alex Ferguson.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!