Msimu
uliopita Arsenal ilimaliza msimu ikiwa kwenye kiwango cha juu,
ikishinda me chi mfululizo ili kujihakikishia nafasi ya kushiriki
Champions League. Jambo moja ambalo limekuwa likiangusha Arsenal kwa
misimu kadhaa iliyopita - ni kupata point chache kutoka vilabu vyenza
vya Top 4. Arsenal ilichukua jumla ya point 2 tu kati ya 18, walifungwa
me chi 4, wakitoa sare mara mbili na hawakushinda mchezo hata moja dhidi
ya Man United, Chelsea, na Man City. Je hii inajirudia pia msimu huh na
itaigharimu Arsenal na ndoto yake ya kutwaa ubingwa?
Kama
tunavyoona hapo juu fomu ya Arsenal dhidi ya vilabu vinavyoshika nafasi
za juu msimu huu ni sawa sawa tu ilivyokuwa msimu uliopita.
Liverpool,
ambao wamefungwa mechi zao 3 za ugenini dhidi ya timu za juu, ina
pointi 3 tu kutoka kwenye mechi dhidi ya timu za Top 4, pointi hizo
imezipata kutka kwa Arsenal. Jambo la kusikitisha zaidi pamoja na msimu
huu kujirekebisha kidogo kwenye ulinzi lakini Arsenal imeruhusu mabao 11
kwenye mechi mbili dhidi ya Manchester City na Liverpool. Hili ni jambo
la kutia wasiwasi.
Kuna
wasiwasi au mtazamo kwamba timu haijiandai vizuri na michezo dhidi ya
timu kubwa, wanaruhusu mabao mengi. Jambo lingine la kutia shaka safu
yao ya ushambuliaji imefunga mabao manne tu, namba ndogo zaidi miongoni
mwa mechi za timu za top 4. Chelsea wana rekodi nzuri, wameruhusu mabao 3
tu na ndio timu pekee iliyoenda Etihad na kushinda - na kutoka na clean
sheet pia.
Manchester
City wana kikosi kizuri mno na itakuwa vigumu kufungwa watakapoenda
Emirates na Anfield. Chelsea wana mchezo mmoja wa ugenini dhidi ya
Liverpool na mmoja wa home dhidi ya Arsenal. Fomu ya Chelsea dhidi ya
timu za juu ni nzuri sana na chini ya Jose Mourinho wameweza kujua
namna ya kupata matokeo katika mechi kubwa kwa mbinu zozote zile.
Wenger
inabidi ajipange vizuri katika mechi mbili zijazo dhidi ya Manchester
City na Chelsea, endapo watapoteza mechi hizo ni wazi ndoto yao ya
kubeba ubingwa msimu huu itabaki kuwa ndoto.
Arsenal
wana mkusanyiko wa michezo migumu sana katika siku za hivi karibu. Jana
walishindwa kuifunga Man United walio kwenye hali mbaya kabisa,
wakitoka hapo wanaenda kukutana Liverpool kwenye kombe la FA, then
wanaikaribisha Bayern Munich Emirates wiki ijayo, then watakutana na
mahasimu wao Spurs, na Chelsea kisha Everton, huku wakisubiri
kuikaribisha City Emirates.
Mpaka
kufikia mwishoni mwa 3 tunaweza kujua hatma ya Arsenal msimu huu -
watamaliza ukame wa miaka 9 bila kombe au wataingia mwaka wa 10 bila
kuvaa medali.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!