Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia ametangaza kuwa
Moscow itaunga mkono matokeo na uamuzi wowote utakaopatikana kwa mujibu
wa makubaliano ya pande mbili yaani serikali na waasi huko Syria.
Gennady Gatilov amesema kuwa kuundwa serikali ya mpito na kupambana na
ugaidi huko Syria ni masuala mawili tafauti na yote ni muhimu. Amesema
mambo hayo yanapasa kujadiliwa kwa kina kwenye mazungumzo ya pande hizo
mbili. Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Rusia amesisitiza kuwa ujumbe
unaoiwakilisha serikali ya Syria kwenye mazungumzo hayo hauna azma ya
kujiondoa katika mazungumzo ya Geneva na kwamba jambo hilo
linathibitisha azma ya Damascus ya kutaka kutatuliwa hitilafu zilizopo.
Hii ni katika hali ambayo Wendy Sherman Naibu Waziri wa
Mashauri ya Kigeni wa Marekani amedai kuwa, Washington na Moscow
zimekubaliana kutekelezwa vipengee vya mkutano wa Geneva 1.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!