Umoja wa Ulaya unajiandaa kutuma wanajeshi karibu elfu moja huko
Jamhuri ya Afrika ya Kati. Mkuu wa Siasa za Nje wa Umoja wa Ulaya Bi
Catherine Ashton ameyasema hayo baada ya kikao cha Baraza la Usalama la
Umoja wa Mataifa hapo jana. Ashton amesema, hadi sasa umoja huo una
zaidi ya wanajeshi 500 nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati na kwamba EU
inatafuta namna ya kuzidisha mara mbili idadi hiyo ya wanajeshi.
Mkuu wa Siasa za Nje wa Umoja wa Ulaya amesema anatumai kuwa nyongeza hiyo ya wanashi wataelekea Jamhuri ya Afrika ya Kati hivi karibuni. Ofisi ya Rais Francois Hollande wa Ufaransa pia imeeleza hapo jana kupitia taarifa yake kwamba Paris inapanga kuimarisha vikosi vyake vilivyoko Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa kutuma wanajeshi wengine 400 katika koloni hilo la zamani la Ufaransa.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!