Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza amesema, ana wasiwasi na
hatua ya baadhi ya raia wa nchi hiyo ya kuelekea nchini Syria kwa ajili
ya kushiriki katika mapigano. Akihojiwa na kanali ya televisheni ya CNN
ya Marekani, William Hague amesema kuwa, kwa mujibu wa ripoti zisizo na
shaka yoyote, mamia ya raia wa Uingereza na wa nchi nyingine za
Magharibi wanapigana bega kwa bega na magaidi huko Syria. Akiulizwa
swali juu ya uwezekano wa wapiganaji hao wa Uingereza kuondoka huko
Syria na kurejea nchini kwao kwa lengo la kuendeleza mashambulizi ya
kigaidi huko Uingereza, Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo amejibu kwa
kusema kuwa, London itasimama imara kukabiliana na mashambulizi ya
kigaidi yanayoweza kufanywa na watu hao.
Hague ameashiria kuweko uwezekano wa kuzuiwa kurejea magaidi hao nchini Uingereza na kuchukuliwa hatua kali za kiusalama na kueleza kuwa, wapiganaji hao ni hatari kwa usalama wa Uingereza. Nchi za Magharibi ikiwemo Uingereza, katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita zimekuwa zikiyaunga mkono kwa hali na mali makundi ya kigaidi na yale yenye misimamo ya kufurutu mipaka huko Syria.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!